TAKWIMU ZA AJALI NA MAKOSA YA BARABARANI, DISEMBA 2025 image

TAKWIMU ZA AJALI NA MAKOSA YA BARABARANI, DISEMBA 2025

Lengo kuu la kutolewa toleo hili ni kutoa taarifa za ajali na makosa ya barabarani za ndani ya Zanzibar. Taarifa hizi ni muhimu na hutumika na wapangaji, watunga sera, watoa maamuzi na wasimamizi wa sheria.

Jumla ya ajali 28 zimeripotiwa mwezi Disemba, 2025. Wilaya ya Kati imeripotiwa kuwa na ajali zaidi, ajali saba (7) sawa na asilimia 25.0 ukilinganisha na wilaya nyingine.

Published on December 19, 2025