TOLEO LA TAKWIMU ZA UDHALILISHAJI MWEZI, AGOSTI 2026 image

TOLEO LA TAKWIMU ZA UDHALILISHAJI MWEZI, AGOSTI 2026

Jumla ya matukio 157 ya ukatili na udhalilishaji wa kijinsia yameripotiwa mwezi wa Agosti, 2026 ambapo
waathirika walikuwa 157. Waathirika wengi walikuwa watoto (waathirika 136 sawa na asilimia 86.6),
wakifuatiwa na wanawake 18 (asilimia 11.5) na wanaume walikuwa watatu (3) sawa na asilimia 1.9.
Miongoni mwa waathirika watoto 136, wasichana walikuwa 116 (asilimia 85.3) na wavulana walikuwa 20
sawa na asilimia 14.7 ya waathirika watoto

Published on October 01, 2026