Jumla ya matukio 129 ya ukatili na udhalilishaji wa kijinsia yameripotiwa mwezi wa Aprili, 2026 ambapo waathirika walikuwa 129. Waathirika wengi walikuwa watoto (waathirika 108 sawa na asilimia 83.7), wakifuatiwa na wanawake 19 (asilimia 14.7) na wanaume wawili (2) sawa na asilimia 1.6. Miongoni mwa waathirika watoto 108, wasichana walikuwa 93 (asilimia 86.1) na wavulana walikuwa 15 sawa na asilimia 13.9 ya waathirika watoto wote.
Published on May 29, 2026