Jumla ya matukio 103 ya ukatili na udhalilishaji wa kijinsia yameripotiwa mwezi wa Machi, 2026 ambapo waathirika walikuwa 103. Waathirika wengi walikuwa watoto (waathirika 84 sawa na asilimia 81.6), wakifuatiwa na wanawake 17 (asilimia 16.5) na wanaume wawili (2) sawa na asilimia 1.9 Miongoni mwa waathirika watoto 84, wasichana walikuwa 75 (asilimia 89.3 ) na wavulana walikuwa tisa (9) sawa na asilimia 10.7 ya waathirika watoto wote.
Published on April 29, 2026