Jumla ya matukio 113 ya ukatili na udhalilishaji wa kijinsia yameripotiwa mwezi wa Januari, 2026 ambapo waathirika walikuwa 113. Waathirika wengi walikuwa watoto (waathirika 91 sawa na asilimia 80.5), wakifuatiwa na wanawake 20 (asilimia 17.7) na wanaume wawili (2) sawa na asilimia 1.8 Miongoni mwa waathirika watoto 91, wasichana walikuwa 79 (asilimia 86.8) na wavulana walikuwa 12 (asilimia 13.2).
Published on March 03, 2026