TOLEO LA TAKWIMU ZA AJALI BARABARANI MWEZI, AGOSTI 2026
Ajali za Barabarani
Jumla ya ajali 28 zimeripotiwa mwezi Agosti, 2026. Wilaya ya Kaskazini ‘A’ na Kaskazini ‘B’ zimeripotiwa
kuwa na ajali zaidi, ajali tano (5) sawa na asilimia 17.9 kwa kila wilaya ukilinganisha na wilaya nyingine.
Idadi ya ajali za barabarani zilizotokea kwa mwezi Agosti, 2026 zimepungua kwa asilimia 3.4 na kufikia ajali 28
kutoka ajali 29 zilizoripotiwa mwezi Julai 2026.
Mwezi wa Agosti 2026, wilaya ya Kaskazini ‘A’ na Kaskazini ‘B’ zimeripotiwa kuwa na ajali zaidi, ajali tano (5)
kwa kila wilaya ikilinganishwa na mwezi wa Julai 2026 ambapo wilaya ya Kaskazini ‘B’ na Magharibi ‘B’ ziliripotiwa
kuwa na ajali zaidi (ajali 6 kwa kila wilaya).
Published on September 16, 2026
Welcome to OCGS
🌟 Welcome to OCGS! 🌟
Stay updated with the latest news and reports directly from OCGS. Subscribe now to receive timely notifications and ensure you never miss out on important releases. We're excited to have you join our community!