TOLEO LA TAKWIMU ZA AJALI BARABARANI MWEZI, JULAI 2026 image

TOLEO LA TAKWIMU ZA AJALI BARABARANI MWEZI, JULAI 2026

Jumla ya ajali 29 zimeripotiwa mwezi Julai, 2026. Wilaya ya Kaskazini ‘B’ na Magharibi ‘B’ zimeripotiwa
kuwa na ajali zaidi, ajali sita (6) sawa na asilimia 20.7 kwa kila wilaya ukilinganisha na wilaya nyingine

Idadi ya ajali za barabarani zilizotokea kwa mwezi Julai, 2026 zimeongezeka kwa asilimia 7.4 na kufikia ajali 29
kutoka ajali 27 zilizoripotiwa mwezi Juni 2026.

Mwezi wa Julai 2026, wilaya ya Kaskazini ‘B’ na Magharibi ‘B’ zimeripotiwa kuwa na ajali zaidi, ajali sita (6) kwa
kila wilaya ikilinganishwa na mwezi wa Juni 2026 ambapo wilaya ya Kaskazini ‘A’ iliripotiwa kuwa na ajali zaidi
(ajali 8).


Published on August 11, 2026