Jumla ya ajali 29 zimeripotiwa mwezi Septemba,2026. Wilaya ya Kati na Magharibi ‘B’ zimeripotiwa kuwa na ajali zaidi, ajali sita (6) sawa na asilimia 20.7 kwa kila wilaya ukilinganisha na wilaya nyingine.
Idadi ya
ajali za barabarani zilizotokea kwa mwezi Septemba, 2026 zimeongezeka kwa
asilimia 3.6 na kufikia ajali 29 kutoka ajali 28 zilizoripotiwa mwezi Agosti
2026.
Mwezi wa Septemba 2026, wilaya ya Kati na Magharibi ‘B’ zimeripotiwa kuwa na ajali zaidi, ajali sita (6) kwa kila wilaya ikilinganishwa na mwezi wa Agosti 2026 ambapo ya
Kaskazini ‘A’ na Kaskazini ‘B’ zimeripotiwa kuwa na ajali zaidi, ajali tano (5) kwa kila wilaya.
Published on October 15, 2026