Lengo kuu la kutolewa toleo hili ni kutoa taarifa za udhalilishaji wa kijinsia ndani ya Zanzibar. Taarifa hizi
ni muhimu na hutumiwa na wapangaji, watunga sera na watoa maamuzi.
Jumla ya matukio 148 ya ukatili na udhalilishaji wa kijinsia yameripotiwa mwezi wa Septemba, 2026
ambapo waathirika walikuwa 148. Waathirika wengi walikuwa watoto (waathirika 123 sawa na asilimia
83.1), wakifuatiwa na wanawake 21 (asilimia 14.2) na wanaume walikuwa wanne (4) sawa na asilimia 2.7.
Miongoni mwa waathirika watoto 136, wasichana walikuwa 116 (asilimia 85.3) na wavulana walikuwa 20
sawa na asilimia 14.7 ya waathirika watoto.
Published on October 23, 2026